Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 89

Zaburi 89:6-25

Help us?
Click on verse(s) to share them!
6Maana ni nani katika mbingu aweza kulinganishwa na Yahwe? Ambaye kati ya wana wa miungu ni kama Yahwe?
7Ni Mungu anaye heshimiwa sana katika baraza la watakatifu naye ni wakutisha kati ya wote wanao mzunguka.
8Yahwe, Mungu wa majeshi, ni nani aliye na nguvu kama wewe, Yahwe? Kweli yako inakuzunguka.
9Wewe huitawala bahari yenye nguvu; mawimbi yainukapo, wewe huyatuliza.
10Ulimwangamiza Rahabu kama mmoja aliye uliwa. Uliwatawanya adui zako kwa mkono wako wenye nguvu.
11Mbingu ni zako wewe, na nchi pia. Uliiumba dunia na vyote vilivyomo.
12Uliumba kaskazini na kusini. Tabori na Hermoni hulifurahia jina lako.
13una mkono wa uweza na mkono wenye nguvu, na mkono wako wa kuume uko juu.
14Haki na hukumu ni msingi wa kiti chako. Uaminifu wa agano lako na uaminifu huja mbele zako.
15Wamebarikiwa watu wakuabuduo wewe! Yahwe, wanatembea katika nuru ya uso wako.
16Siku zote wanafurahia katika jina lako, na katika haki yako wanakutukuza wewe.
17Wewe ni fahari ya nguvu zao, na kwa nguvu zako tu washindi.
18Maana ngao zetu ni za kwako Yahwe; mfalme wetu ni wa Mtakatifu wa Israeli.
19Muda mrefu uliopita ulizungumza na waaminfu wako katika maono; ulisema, “Nimeweka taji juu ya mwenye nguvu; nimemuinua aliyechaguliwa kutoka kati ya watu.
20Nimemchagua Daudi mtumishi wangu; kwa mafuta yangu matakatifu nimempaka yeye.
21Mkono wangu utamsaidia yeye; mkono wangu utamtia nguvu.
22Hakuna adui atakaye mdanganya; hakuna mwana wa uovu atakaye muonea.
23Nitawaangamiza adui zake mbele yake; nitawaua wale wamchukiao.
24Kweli yangu na uaminifu wa agano vitakuwa pamoja naye; kupitia jina langu atakuwa mshindi.
25Nitaweka mkono wake juu ya bahari na mkono wake wa kuume juu ya mito.

Read Zaburi 89Zaburi 89
Compare Zaburi 89:6-25Zaburi 89:6-25