1Nitimba sifa za matendo ya uaminifu wa agano milele. Nitatangaza kweli yako kwa vizazi vijavyo.
2Maana nimesema, “Uaminifu wa agano umeimarishwa milele; na kweli yako umeiimarisha mbinguni.”
3“Nimefanya agano na wateule wangu, nimeapa kiapo kwa Daudi mtumishi wangu.
4Nitauimarisha uzao wako milele, na nitauimarisha utawala wako vizazi vyote.” Selah
5Mbingu husifu maajabu yako, Yahwe; kweli yako inasifiwa katika kusanyiko la watakatifu.
6Maana ni nani katika mbingu aweza kulinganishwa na Yahwe? Ambaye kati ya wana wa miungu ni kama Yahwe?
7Ni Mungu anaye heshimiwa sana katika baraza la watakatifu naye ni wakutisha kati ya wote wanao mzunguka.
8Yahwe, Mungu wa majeshi, ni nani aliye na nguvu kama wewe, Yahwe? Kweli yako inakuzunguka.
9Wewe huitawala bahari yenye nguvu; mawimbi yainukapo, wewe huyatuliza.
10Ulimwangamiza Rahabu kama mmoja aliye uliwa. Uliwatawanya adui zako kwa mkono wako wenye nguvu.
11Mbingu ni zako wewe, na nchi pia. Uliiumba dunia na vyote vilivyomo.
12Uliumba kaskazini na kusini. Tabori na Hermoni hulifurahia jina lako.
13una mkono wa uweza na mkono wenye nguvu, na mkono wako wa kuume uko juu.
14Haki na hukumu ni msingi wa kiti chako. Uaminifu wa agano lako na uaminifu huja mbele zako.
15Wamebarikiwa watu wakuabuduo wewe! Yahwe, wanatembea katika nuru ya uso wako.
16Siku zote wanafurahia katika jina lako, na katika haki yako wanakutukuza wewe.
17Wewe ni fahari ya nguvu zao, na kwa nguvu zako tu washindi.
18Maana ngao zetu ni za kwako Yahwe; mfalme wetu ni wa Mtakatifu wa Israeli.
19Muda mrefu uliopita ulizungumza na waaminfu wako katika maono; ulisema, “Nimeweka taji juu ya mwenye nguvu; nimemuinua aliyechaguliwa kutoka kati ya watu.
20Nimemchagua Daudi mtumishi wangu; kwa mafuta yangu matakatifu nimempaka yeye.
21Mkono wangu utamsaidia yeye; mkono wangu utamtia nguvu.
22Hakuna adui atakaye mdanganya; hakuna mwana wa uovu atakaye muonea.