1 Nitimba sifa za matendo ya uaminifu wa agano milele. Nitatangaza kweli yako kwa vizazi vijavyo.
2 Maana nimesema, “Uaminifu wa agano umeimarishwa milele; na kweli yako umeiimarisha mbinguni.”
3 “Nimefanya agano na wateule wangu, nimeapa kiapo kwa Daudi mtumishi wangu.
4 Nitauimarisha uzao wako milele, na nitauimarisha utawala wako vizazi vyote.” Selah
5 Mbingu husifu maajabu yako, Yahwe; kweli yako inasifiwa katika kusanyiko la watakatifu.
6 Maana ni nani katika mbingu aweza kulinganishwa na Yahwe? Ambaye kati ya wana wa miungu ni kama Yahwe?
7 Ni Mungu anaye heshimiwa sana katika baraza la watakatifu naye ni wakutisha kati ya wote wanao mzunguka.
8 Yahwe, Mungu wa majeshi, ni nani aliye na nguvu kama wewe, Yahwe? Kweli yako inakuzunguka.
9 Wewe huitawala bahari yenye nguvu; mawimbi yainukapo, wewe huyatuliza.
10 Ulimwangamiza Rahabu kama mmoja aliye uliwa. Uliwatawanya adui zako kwa mkono wako wenye nguvu.
11 Mbingu ni zako wewe, na nchi pia. Uliiumba dunia na vyote vilivyomo.
12 Uliumba kaskazini na kusini. Tabori na Hermoni hulifurahia jina lako.
13 una mkono wa uweza na mkono wenye nguvu, na mkono wako wa kuume uko juu.
14 Haki na hukumu ni msingi wa kiti chako. Uaminifu wa agano lako na uaminifu huja mbele zako.
15 Wamebarikiwa watu wakuabuduo wewe! Yahwe, wanatembea katika nuru ya uso wako.
16 Siku zote wanafurahia katika jina lako, na katika haki yako wanakutukuza wewe.
17 Wewe ni fahari ya nguvu zao, na kwa nguvu zako tu washindi.
18 Maana ngao zetu ni za kwako Yahwe; mfalme wetu ni wa Mtakatifu wa Israeli.
19 Muda mrefu uliopita ulizungumza na waaminfu wako katika maono; ulisema, “Nimeweka taji juu ya mwenye nguvu; nimemuinua aliyechaguliwa kutoka kati ya watu.
20 Nimemchagua Daudi mtumishi wangu; kwa mafuta yangu matakatifu nimempaka yeye.
21 Mkono wangu utamsaidia yeye; mkono wangu utamtia nguvu.
22 Hakuna adui atakaye mdanganya; hakuna mwana wa uovu atakaye muonea.