5Je! Utaendelea kuwa na hasira juu yetu milele? utadumisha hasira kizazi chote kijacho?
6Je, hautatuhuisha tena? Kisha watu wako watafurahia katika wewe.
7Utuoneshe sisi uaminifu wa agano lako, Yahwe, utupe sisi wokovu wako.
8Nitasikiliza yale Yahwe Mungu asemayo, maana yeye atafanya amani pamoja na watu wake, wafuasi wake waminifu. Lakini lazima wasirudi tena katika njia za kipumbavu.