2Tazama, adui zako wanafanya vurugu, na wale wakuchukiao wameinua vichwa vyao.
3Wanafanya hila juu ya watu wako na kwa pamoja kupanga njama dhidi ya wale uwalindao. Wamesema,
4“Njoni na tuwaangamize wao kama taifa. Kisha jina la Israeli halitakumbukwa.”
5Wamepanga njama pamoja wakiwa na mkakati mmoja; wamefanya muungano dhidi yako.
6Hii inajumuisha hema za Edomu na Waishmaeli, na watu wa Moabu na Wahagari, ambao wamepanga njama pamoja nao
7Gebal, Amoni, Amaleki; pia inajumuisha Filisti na wenyeji wa Tiro.
8Ashuri pia ameshirikina nao; wanawasaidia wana wa Lutu. Serah
9Ufanye kwao kama ulivyofanya kwa Midiani, kama ulivyofanya kwa Sisera na kwa Yabini kwenye Mto Kishoni.
10Waliangamizwa kule Endori na wakawa kama mbolea juu ya chi.
11Uvifanye vyeo vyao kama Oreb na Zeeb, na wakuu wao wote kama Zeba na Zalmuna.
12Wao walisema, natujimilikishe malisho ya Mungu.”
13Ee Mungu wangu, uwafanye kama mavumbi ya kisulisuli, kama makapi mbele ya upepo,
14Kama moto uteketezao msitu, na kama miali ya moto iwakayo milimani.
15Uwafuatie kwa tufani yako, na kuwafadhaisha kwa dhoruba yako.
16Uwajaze nyuso zao kwa aibu ili kwamba waweze kulitafuta jina lako, Yahwe.
17Nao waaibishwe na kufadhaishwa milele; waangamizwe katika aibu.