11Nilipoteneneza mavazi ya gunia, nikawa kituko kwao.
12Wale wakaao katika lango la mji huniseng'enya; mimi ni wimbo wa walevi.
13Lakini kwangu mimi, maombi yangu ni kwako, Yahwe, wakati ambao wewe utayapokea; unijibu katika uaminifu wa wokovu wako.
14Unitoe matopeni, na usiniache nizame; uniondoe mbali na wale wanaonichukia na uniokoe katika kina cha maji.
15Usiache mafuliko ya maji yanielemee, wala kina kisinimeze. Usiache mdomo wa shimo unimeze.
16Unijibu, Yahwe, maana uaminifu wa agano lako ni mwema; kwa maana rehema zako kwangu ni nyingi, unigeukie.
17Usiufiche uso wako mbali na mtumishi wako, maana niko katika dhiki; unijibu haraka.
18Uje kwangu na unikomboe. Kwa sababu ya adui zangu, uwe fidia yangu.