1Mungu ainuke, maadui zake watawanyike; pia wale wamchukiao wakimbie mbele zake.
2Kama moshi uondoshwavyo, hivyo uwaondoshe wao; kama nta iyeyukavo mbele ya moto, hivyo waovu waangamizwe uweponi mwa Mungu.
3Bali wenye haki wafurahi; washangilie mbele za Mungu; washangilie na kufurahi.
4Mwimbieni Mungu! Lisifuni jina lake! Msifuni yule aendeshaye farasi kwenye tambarare ya bonde la Mto Yordani! Yahwe ni jina lake! Shangilieni mbele zake!