1Mungu atuhurumie sisi na kutubariki na kufanya nuru ya uso wake ituangazie Selah
2ili kwamba njia zako zijulikane nchi yote, wokovu wako kati ya mataifa yote.
3Watu wakusifu wewe, Mungu; watu wote wakusifu wewe.
4Oh, mataifa wafurahi na na kuimba kwa furaha, maana utawahukumu watu kwa haki na kuwaongoza mataifa walioko duniani.
5Watu wakushukuru wewe, Mungu; watu wote wakusifu wewe.