5Katika haki wewe utatujibu sisi kwa kufanya mambo ya ajabu, Mungu wa wokovu wetu; wewe ambaye ni ujasiri wa mwisho wote wa nchi na wa wale walio mbali toka pande za bahari.
6Kwa manaa ni wewe ndiye uliyeifanya milima imara, wewe ambaye umefungwa mkanda wa uweza.
7Ni wewe unyamazishaye ngurumo za baharini; ngurumo za mawimbi yake, na vurugu za watu.