2Kutokea mwisho wa nchi nitakuita wewe wakati moyo wangu umeelemewa; uniongoze kwenye mwamba ulio juu kuliko mimi.
3Maana wewe umekuwa kimbilio langu la usalama, nguzo imara dhidi ya adui.
4Uniache niishi hemani mwako milele! Nipate kimbilio salama chini ya makazi ya mbawa zako. Selah
5Kwa kuwa wewe, Mungu, umesikia viapo vyangu, wewe umenipa mimi urithi wa wale wanao liheshimu jina lako.