7Unisafishe kwa hisopo, nami nitakuwa safi; unioshe, nami nitakuwa mweupe kuliko theluji.
8Unifanye kusikia furaha na shangwe ili kwamba mifupa ulioivunja ifurahi.
9Uufiche uso wako mbali na dhambi zangu na uyafute maovu yangu yote.
10Uniumbie moyo safi, Mungu, na uifanye upya roho ya haki ndani yangu.
11Usiniondoe uweponi mwako, na usimuondoe roho Mtakatifu ndani yangu.