1Unirehemu, Mungu, kwa sababu ya uaminifu wa agano lako; kwa ajili ya wingi wa matendo yako ya rehema, uyafute makosa yangu.
2Unioshe kabisa uovu wangu na unisafishe dhambi zangu.
3Kwa maana ninayajua makosa yangu, na dhambi yangu iko mbele yako siku zote.
4Dhidi yako, wewe pekee, nimetenda dhambi na kufanya uovu mbele ya macho yako; uko sawa usemapo; wewe uko sahahi utoapo hukumu.