1Mungu, Mwenye nguvu, Yahwe, amenena naye aliita nchi toka mawio ya jua mpaka machweo yake.
2Tokea Sayuni, Mungu ameangaza, ukamilifu wa uzuri.
3Mungu wetu huja naye hakai kimya; mbele yake moto hula, na kuna dhoruba kubwa karibu naye.
4Yeye huziita mbingu zilizo juu na nchi ili kwamba aweze kuwahukumu watu wake:
5Kwa pamoja kusanyikeni waaminifu wangu kwangu, wale waliofanya nami agano kwa sadaka.”
6Mbingu zitatangaza haki yake, kwa maana Mungu mwenyewe ndiye jaji. Serah
7Sikilizeni, watu wangu, nami nitazungumza; mimi ni Mungu, Mungu wenu.
8Sitawakaripia ninyi kwa ajili ya sadaka zenu; sadaka zenu za kuteketeza ziko nami siku zote.
9Sitachukua ng'ombe katika nyumba yenu, wala beberu katika mazizi yenu.
10Kwa maana kila mnyama wa msituni ni wangu, nao ng'ombe kwenye milima elfu ni wangu.
11Ninawajua ndege wa mlimani, na wanyama pori katika shamba ni wangu.
12Kama ningekuwa na njaa, nisingewaambia ninyi; maana ulimwengu ni wangu, na vyote vilivyomo.