14Kama kondoo wamechaguliwa kwa ajili ya kuzimu na kifo kitakuwa mchungaji wao. Nao watatawaliwa na wenye haki ifikapo asubuhi, na miili yao italiwa kuzimuni, wakiwa hawana afasi ya kuishi kwa ajili yao.
15Bali Mungu ataufufua uhai wangu kutoka katika nguvu ya kuzimu; naye atanipokea. Selah
16Msifadhaike mtu awapo tajiri, utukufu wa nyumba yake uongezekapo.