2Hivyo hatutaogopa, hata kama dunia italazimika kubadilika, hata kama milima italazimika kutetemeka na kuangukia kwenye mtima wa bahari, hata kama maji yatavuma kwa kishindo kikuu,
3hata kama milima itatetemeka kwa vurugu ya maji. Selah
4Kuna mto, mikondo yake huufanya mji wa Mungu kufurahi, mahali patakatifu pa hema ya Aliye Juu.
5Mungu yuko katikati yake; naye hatasogezwa; Mungu atamsaidia, naye atafanya hivyo asubuhi na mapema.
6Mataifa yalikasirika na falme zikataharuki; yeye alipaza sauti yake, na nchi ikayeyuka.
7Yahwe wa majeshi yuko pamoja nasi; Mungu wa Yakobo ni kimbilio letu la usalama. Selah
8Njoni, mtazame matendo ya Yahwe, uharibifu alioufanya juu ya nchi.
9Anaisitisha vita kwenye nchi; yeye anauvunja upinde na kuikata vipande vipande mishale; anazichoma ngao.
10Mkae kimya na mjue kuwa mimi ni Mungu; nitainuliwa juu ya nchi.
11Mungu wa majeshi yuko pamoja nasi; Mungu wa Yakobo ni kimbilio letu la usalama. Serah