3Mwili wangu wote unaumwa kwa sababu ya hasira yako; kwa sababu ya dhambi zangu mifupa yangu haina afya.
4Kwa maana maovu yangu yamenielemea; yamekuwa mzigo mzito kwangu.
5Vidonda vyangu vimeoza na vinanuka kwa sababu ya upumbavu wa dhambi zangu.
6Nimepindika na kuwa mnyonge kila siku; ninaenenda katika maombolezo siku zote.
7Kwa maana ndani yangu, ninaungua; hakuna afya katika mwili wangu.
8Nimedhohofika na kulemewa sana; ninaugua kwa sababu ya dhiki yangu.
9Bwana, wewe unaielewa shauku ya ndani kabisa ya moyo wangu, na kuugua kwangu hakujifichika kwako.
10Moyo wangu unapwita pwita, nguvu zangu zinaniisha, macho yangu yanafifia.
11Marafiki na ndugu zangu wamenitenga kwa sababu ya hali; majirani zangu hukaa mbali nami.
12Wale wanaoutafuta uhai wangu hutega mitego kwa ajili yangu. Wao ambao hutafuta kunidhuru huongea maneno ya uharibifu na husema maneno ya uongo siku nzima.
13Lakini, niko kama mtu kiziwi na sisikii lolote; niko kama mtu bubu ambaye hasemi lolote.