Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 36

Zaburi 36:6-12

Help us?
Click on verse(s) to share them!
6Haki yako ni kama milima ya Mungu; hukumu yako ni kama kina kirefu. Yahwe, wewe huwahifadhi wote wanadamu na wanyama.
7Ni jinsi gani uaminifu wa aganao lako ni wa thamani, Mungu! Watu hukimbilia usalama chini ya uvuli wa mbawa zako.
8Nao watatoshelezwa tele na utajiri wa chakula nyumbani mwako; utawafanya wanywe kutoka katika mto wa baraka zako za thamani.
9Kwa kuwa mna chemichemi ya uzima; na katika mwanga wako tutaiona nuru.
10Uupanue uaminifu wa agano lako kikamilifu kwa wale wanao kujua wewe, ulinzi wako uwe juu ya wanyoofu wa moyo.
11Usiuache mguu wa mwenye kiburi unisogelee. Usiiache mkono wa mwovu unitoweshe.
12Kule wafanyao maovu wameanguka; wameharibiwa hawawezi kuinuka.

Read Zaburi 36Zaburi 36
Compare Zaburi 36:6-12Zaburi 36:6-12