Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 35

Zaburi 35:9-28

Help us?
Click on verse(s) to share them!
9Bali mimi nitakuwa nafuraha ndani ya Yahwe na ndani ya wokovu wake.
10Mifupa yangu yote itasema, “Yahwe, ni nani kama wewe, uokoaye walio onewa mkononi mwa walio na nguvu kuwazidi wao na masikini na wahitaji mkononi mwa wale wanaojaribu kuwaibia?”
11Mashahidi wa uongo wamesimama; wananishitakia uongo.
12Kwa ajili ya wema wananilipa mabaya. Nina huzuni nyingi.
13Lakini, walipokuwa akiugua, nilivaa magunia; nilifunga kwa ajili yao huku kichwa changu kikiinamia kifuani kwangu.
14Nilienenda katika huzuni kana kwamba walikuwa ni ndugu zangu; niliinama chini nikiomboleza kana kwamba ni kwa ajili ya mama yangu.
15Bali mimi nilipokuwa mashakani, walifurahi sana na kukutanika pamoja; walikutanika pamoja kinyume na mimi, nami nilishangazwa nao. Walinirarua bila kuacha.
16Kwa dharau kabisa walinidhihaki; walinisagia meno yao.
17Bwana, mpaka lini utaendelea kutazama? uiokoe roho yangu na mashambulizi yao ya maagamizi uyaokoe maisha yangu na simba.
18Nami nitakushukuru wewe katika kusanyiko kubwa; nitakusifu kati ya watu wengi.
19Usiwaache maadui zangu wadanganyifu kufurahi juu yangu; usiwaache waendelee na mipango yao ya uovu.
20Kwa maana hawaongei amani, bali wanabuni maneno ya uongo kwa wale wanaoishi kwa amani katika ardhi yetu.
21Midomo yao inapaza sauti ikinishtaki; wakisema, Aha, Aha, macho yetu yameona.”
22Yahwe wewe umeona, usikae kimya; Bwana, usiwe mbali nami.
23Inuka mwenyewe na usimame kunitetea; Mungu wangu na Bwana wangu, unitetee.
24Kwa sabababu ya haki yako, Yahwe Mungu wangu, unitetee; usiwaache wafurahi kwa ajili yangu.
25Usiwaache waseme mioyoni mwao, “Aha, tumepata tulicho kihitaji.” Usiwaache waseme, tumemmeza.”
26Uwaaibishe na kuwa fendhehesha wale wanaotaka kunidhuru. Wale wote wanao ni dhihaki wafunikwe kwa aibu na kudharauliwa.
27Nao wote wanao tamani kudhihirishwa kwangu washangilie na wafurahi; siku zote waseme, “Usifiwe Yahwe, yeye ajifurahishaye katika mafanikio ya mtumishi wake.
28Kisha nitatangaza matendo yako ya haki na kukusifu wewe wakati wote.

Read Zaburi 35Zaburi 35
Compare Zaburi 35:9-28Zaburi 35:9-28