1Yahwe, uwashughulikie wale wanao nishughulikia mimi; upigane nao wanao pigana nami.
2Uikamate ngao yako ndogo na ngao kubwa; inuka unisaidie.
3Uutumie mkuki wako na shoka lako la vita kwa wale wanao nifukuzia; uuambie moyo wangu, “Mimi ni wokovu wako.”