8Basi ulimwengu wote umwogope Yahwe; wenyeji wote wa ulimwengu wamuhofu yeye.
9Kwa maana yeye alisema, na ikafanyika; aliamuru, na ikasimama mahali pake.
10Yahwe huvunja muungano wa mataifa; naye huishinda mipango ya wanadamu.
11Mipango ya Yahwe husimama milele, mipango ya moyo wake ni kwa ajili ya vizazi vyote.
12Limebarikiwa taifa ambalo Mungu wao ni Yahwe, watu ambao yeye amewachagua kama warithi wake.
13Yahwe anatazama kutoka mbinguni; yeye huona watu wote.
14Kutokea mahali ambapo yeye anaishi, huwatazama wote waishio juu ya nchi.
15Yeye anaye iumba mioyo yao na kuyaona matendo yao yote.