1Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi ya Daudi. In wewe, Yahwe, nakimbilia usalama; usiniache niaibishwe. Katika haki yako uniokoe.
2Unisikie; uniokoe haraka; uwe mwamba wangu wa usalama, ngome ya kuniokoa.
3Kwa kuwa wewe ni mwamba wangu na ngome yangu; kwa hiyo kwa ajili ya jina lako, uniongoze na unielekeze.
4Unitoe katika mtego ambao wameuficha kwa ajili yangu, kwa kuwa wewe ni usalama wangu.
5Mikononi mwako naikabidhi roho yangu; nawe utaniokoa, Yahwe, mwenye kuaminika.
6Ninawachukia wale wanaotumikia miungu isiyo na maana, bali ninaamini katika Yahwe.
7Nitafurahi na kushangilia katika uaminifu wa agano lako, kwa kuwa uliyaona mateso yangu; wewe uliijua dhiki ya moyo wangu.
8Wewe haujaniweka kwenye mkono wa maadui zangu. Nawe umeiweka miguu yangu mahali pa wazi papana.