Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 27

Zaburi 27:5-9

Help us?
Click on verse(s) to share them!
5Kwa kuwa katika siku ya shida atanificha nyumbani mwake; atanificha katika mfuniko wa hema lake. Yeye ataniinua juu ya mwamba!
6Kisha kichwa changu kitainuliwa juu ya maadui wote wanizungukao, nami nitatoa sadaka ya furaha hemani mwake! Nitaimba na kutunga nyimbo kwa Yahwe!
7Sikia, sauti yangu nikuitapo, Yahwe! Unihurumie, na unijibu!
8Moyo wangu huongea kuhusu wewe, “Utafute uso wake!” Nami nautafuta uso wako, Yahwe!
9Usiufiche uso wako mbali na mimi; usinikasirikie mimi mtumishi wako! Wewe umekuwa msaada wangu; usiniache wala kunitelekeza, Mungu wa wokovu wangu!

Read Zaburi 27Zaburi 27
Compare Zaburi 27:5-9Zaburi 27:5-9