9Kwa kuwa wewe ulinileta kutoka tumboni; wewe ulinifanya nikuamini wewe wakati nikiwa nanyonya matiti ya mama yangu.
10Nimekwisha tupwa kwako wewe tokea tumboni; wewe ni Mungu wangu tangu nikiwa tumboni mwa mama yangu!
11Usiwe mbali na mimi, kwa kuwa shida ikaribu; hayupo hata mmoja wa kusaidia.
12Maksai wengi wananizunguka mimi; maksai wenye nguvu ya Bashan wananizunguka mimi.
13Wao wanafungua midomo yao kwangu kama simba aungurumaye akirarua windo lake.
14Ninamwagwa nje kama maji, na mifupa yangu yote imeteguka. Moyo wangu ni kama nta; nao unayeyuka ndani ya sehemu zangu za ndani.
15Nguvu zangu zimekaushwa kama kipande cha ufinyanzi; ulimi wangu unanata juu ya mdomo wangu. Wewe umenilaza mimi katika vumbi la mauti.
16Kwa maana mbwa wamenizunguka; kundi la watu waovu limenizunguka; wamenitoboa mikono yangu na miguu yangu.
17Nami ninaweza kuihesabu mifupa yangu. Wao wananitazama na kunishangaa.
18Wao wanagawa mavazi yangu kati yao wenyewe, wanapiga kura kwa ajili ya mavazi yangu.
19Usiwe mbali, Yahwe; tafadhali harakisha kunisaidia mimi, nguvu yangu!
20Uiokoe roho yangu na upanga, maisha yangu mwenyewe na makucha ya mbwa mwitu.
21Uniokoe na mdomo wa simba; uniokoe na mapembe ya ng'ombe wa porini.
22Nami nitalitangaza jina lako kwa ndugu zangu; katikati ya kusanyiko la watu nitakusifu wewe.
23Ninyi mnao mwogopa Yahwe, msifuni yeye! Ninyi nyote kizazi cha Yakobo, muheshimuni yeye! Simameni katika hofu yake, ninyi nyote kizazi cha Israeli!
24Kwa kuwa haja dharau au kuchukia mateso ya aliye taabishwa; Yahwe hajamficha uso wake yeye; pindi wale walio taabishwa walipo mlilia yeye, yeye alisikia.
25Yahwe, katika kusanyiko la watu wako nitakusifu kwa yale uliyo tenda; nami nitatimiza nadhiri zangu mbele ya wale wanao muhofu yeye.
26Walio onewa watakula na kutosheka; wale ambao humtafuta Yahwe watamsifu yeye. Mioyo yenu iishi milele.
27Watu wote wa duniani watakumbuka na kumrudia Yahwe; familia zote za mataifa watapiga magoti chini mbele yako.
28Kwa kuwa utawala ni wa Yahwe; yeye ni mtawala wa mataifa.
29Watu wote wa duniani waliofanikiwa wata sherekea na wata abudu; wale wote washukao katika mavumbi watapiga magoti mbele zake, wale ambao hawawezi kulinda maisha yao wenyewe.
30Kizazi kijacho kitamtumikia yeye; wao watakiambia kizazi kinachofuatia kuhusu Bwana.