1Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi ya Daudi. Mungu akusaidie wakati wa shida; na jina la Mungu wa Yakobo likulinde
2na kutuma msaada kutoka mahali patakatifu kwa ajili ya kukutegemeza wewe kutoka Sayuni.
3Naye akumbuke sadaka yako yote na kuipokea sadaka ya kuteketezwa.
4Naye akujalie haja za moyo wako na kutimiza mipango yako yote.