5Kamba za kuzimu zilinizunguka; mitego ya mauti ilininasa.
6dhiki yangu nilimuita Yahwe; Niliita msaada kwa Mungu. Naye alisikia sauti yangu kutoka hekaluni mwake; kuita kwangu msaada kulienda mpaka uweponi mwake; na kuingia masikioni pake.
7Kisha nchi ikatikisika na kutetemeka; misingi ya milima pia ilitetemeka na kutikiswa kwa sababu Mungu alikuwa amekasirika.
8Moshi ulifuka kutoka kwenye pua zake, na moto mkali ulitokea mdomoni mwake. Makaa yaliwashwa kwa moto huo.
9Yeye alizifunua mbingu na alishuka chini, na giza nene lilikuwa chini ya miguu yake.
10Alipanda kwenye kerubi na akaruka; alinyiririka kwenye mabawa ya upepo.
11Yahwe alilifanya giza kuwa hema likimzunguka yeye, wingu la mvua zito katika mbingu.
12Mawe ya barafu na makaa ya moto yalianguka kutoka katika mwangaza kabla yake.