2Uthibitisho wangu na uje kutoka uweponi mwako; macho yako na yaone kile kilicho sahihi!
3Kama utaujaribu moyo wangu, kama utakuja kwangu wakati wa usiku, wewe utanitakasa na hautapata mipango yeyote ya uovu; mdomo wangu hautavunja sheria.
4Kama kwa matendo ya binadamu, ni katika neno la midomo yako ya kuwa nimejiepusha na njia za wahalifu.
5Mwenendo wangu umeshikila kwa umakini mwenendo wako; miguu yangu haija teleza.
6Nakuita wewe, kwa kuwa unanijibu, Mungu; geizia sikio lako kwangu na usikilize ninapo ongea.