5Amebarikiwa yule ambaye Mungu wa Yakobo ni msaada wake, ambaye tumaini lake liko katika Yahwe Mungu wake.
6Yahwe aliumba mbingu na nchi, bahari, na vyote vilivyomo; huitazama kweli milele.
7Yeye hutekeleza hukumu kwa ajili ya walioonewa na huwapa chakula wenye njaa. Yahwe huwafungua waliofungwa;
8Yahwe huyafungua macho ya kipofu; Yahwe huwainua walioinama; Yahwe huwapenda watu wenye haki.
9Yahwe huwalinda wageni katika nchi; huwainua yatima na wajane, bali huipinga njia ya wasio haki.
10Yahwe atatawala milele, Mungu wako, Sayuni, kwa vizazi vyote. Msifuni Yahwe.