2Ninamsifu Mungu maisha yangu yote; nitamuimbia sifa Mungu wangu ni ngali ni hai.
3Msiweke imani katika wakuu au wanadamu, ambaye katika yeye hamna wokovu.
4Wakati uhai wa pumzi ya mtu unapokoma, hurudi aridhini; siku hiyo mipango yake hufikia mwisho.
5Amebarikiwa yule ambaye Mungu wa Yakobo ni msaada wake, ambaye tumaini lake liko katika Yahwe Mungu wake.
6Yahwe aliumba mbingu na nchi, bahari, na vyote vilivyomo; huitazama kweli milele.
7Yeye hutekeleza hukumu kwa ajili ya walioonewa na huwapa chakula wenye njaa. Yahwe huwafungua waliofungwa;
8Yahwe huyafungua macho ya kipofu; Yahwe huwainua walioinama; Yahwe huwapenda watu wenye haki.