14Yahwe huwategemeza wote waangukao na huwainua wote walioinama chini.
15Macho ya wote yanakungoja wewe; nawe huwapa chakula chao kwa wakati sahihi.
16Huufungua mkono wako na hukidhi haja ya kila kiumbe hai.
17Yahwe ni mwenye haki katika njia zake zote na neema katika yote afanyayo.