2Wewe ni uaminifu wa agano langu na ngome yangu, mnara wangu mrefu na uniokoaye, ngao yangu na yule ambaye katika yeye napata kimbilio, uyatiishaye mataifa chini yangu.
3Ee Yahwe, mtu ni kitu gani hata umtazame au mwana wa mtu hata umfikirie?
4Mtu ni kama pumzi, siku zake ni kama uvuli upitao.
5Ee Yahwe uziinamishe mbingu na ushuke chini, uiguse milima na uifanye kutoa moshi.
6Utume umeme uwatawanye adui zangu; upige mishale yako na uwavuruge.
7Nyosha mkono wako toka juu; uniokoe kutoka katika maji mengi, na kutoka katika mkono wa wageni.
8vinywa vyao hunena uongo, na mkono wao wa kuume ni mkono wa uongo.
9Nitakuimbia wimbo mpya, Mungu; kwa kinanda cha nyuzi kumi nitakuimbia sifa wewe,
10uwapaye wafalme wokovu, uliye muokoa Daudi mtumishi wako dhidi ya upanga wa uovu.
11Uniokoe na unitoe mkononi mwa wageni. Midomo yao huongea uongo, na mkono wao wa kuume ni mkono wa uongo.