1Atukuzwe Yahwe, mwamba wangu, anifundishaye mikono yangu vita na vidole vyangu kupigana.
2Wewe ni uaminifu wa agano langu na ngome yangu, mnara wangu mrefu na uniokoaye, ngao yangu na yule ambaye katika yeye napata kimbilio, uyatiishaye mataifa chini yangu.
3Ee Yahwe, mtu ni kitu gani hata umtazame au mwana wa mtu hata umfikirie?
4Mtu ni kama pumzi, siku zake ni kama uvuli upitao.
5Ee Yahwe uziinamishe mbingu na ushuke chini, uiguse milima na uifanye kutoa moshi.