Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 139

Zaburi 139:1-15

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Ee Yahwe, wewe umenichunguza, na unanijua.
2Wewe unajua nikaapo na niinukapo; unayajua mawazo yangu tokea mbali sana.
3Unachunguza wenendo wangu na kulala kwangu; unazijua njia zangu zote.
4Kabla hakujawa na neno kwenye ulimi wangu, wewe unalijua kabisa, Yahwe.
5Nyuma yangu na mbele yangu unanizunguka na kuniwekea mkono wako.
6Maarifa hayo ni mengi yananizidi mimi; yako juu sana, nami siwezi kuyafikia.
7Niende wapi mbali na roho yako? Niende wapi niukimbie uwepo wako?
8Kama nikipaa mbinguni, uko huko; kama nikifanya kitanda changu Kuzimuni, tazama, uko huko.
9Kama nikipaa kwa mbawa za asubuhi na kwenda kuishi pande za mwisho wa bahari,
10hata huko mkono wako utaniongoza, mkono wako wa kuume utanishika.
11Kama nikisema, “Hakika giza litanifunika, na nuru inizungukayo itakuwa usiku,”
12Hata giza lisingweza kuwa giza kwako. Usiku ungeng'aa kama mchana, maana giza na nuru kwako vinafanana.
13Wewe uliumba sehemu zangu za ndani; uliniumba tumboni mwa mama yangu.
14Nitakusifu, kwa maana nimeumbwa kwa jinsi ya ajabu. Nafsi yangu yalijua hili vizuri sana.
15Mifupa yangu haikusitirika kwako nilipoumbwa kwa siri, nilipoumbwa kwa ustadi pande za chini za nchi.

Read Zaburi 139Zaburi 139
Compare Zaburi 139:1-15Zaburi 139:1-15