Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 138

Zaburi 138:2-7

Help us?
Click on verse(s) to share them!
2Nitasujundu mbele ya hekalu lako takatifu na kulishukuru jina lako kwa ajili ya uaminifu wa agano lako na kwa uaminifu wako. Umelifanya muhimu zaidi neno lako na jina lako kuliko kitu chochote.
3Siku ile niliyo kuita, ulinijibu; ulinitia moyo na kuitia nguvu nafsi yangu.
4Wafalme wote wa nchi watakushukuru wewe, Yahwe, maana watasikia maneno kutoka kinywani mwako.
5Hakika, wataimba kuhusu matendo ya Yahwe, kwa kuwa utukufu wa Yahwe ni mkuu.
6Maana ingawa Yahwe yuko juu, lakini anawajali wanyenyekevu, lakini hawatambui wenye majivuno.
7Nijapopita katikati ya hatari, wewe utauhifadhi uhai wangu; utanyoosha mkono wako dhidi ya hasira ya adui zangu, na mkono wako wa kuume utaniokoa.

Read Zaburi 138Zaburi 138
Compare Zaburi 138:2-7Zaburi 138:2-7