6Chochote Yahwe apendacho, hufanya mbinguni, duniani, katika bahari na katika vilindi vyote.
7Hushusha mawingu kutoka mbali, akifanya mianga ya radi kuongozana na mvua na kuleta upepo toka katika ghala yake.
8Aliua mzaliwa wa kwanza wa Misri, wote wanadamu na wanyama.
9Alituma ishara na maajabu kati yako Misri, dhidi ya Farao na watumishi wake wote.
10Aliwashambulia mataifa mengi na aliua wafalme wenye nguvu,
11Sihoni mfalme wa Waamori na Ogu mfalme wa Bashani na falme zote za Kanaani.
12Alitupatia sisi nchi yao kama urithi, urithi wa Israeli watu wake.
13Jina lako, Yahwe, inadumu milele; Yahwe, kumbukumbu lako vizazi hata vizazi.