5mpaka nitakapopata mahali kwa ajili ya Yahwe, na maskani kwa ajili ya Shujaa wa Yakobo.”
6Tazama tulisikia kuhusu hilo katika Efrata; tuliipata katika konde la Yearimu.
7Tutaingia katika maskani ya Mungu; tutasujudu miguuni pake.
8Inuka, Ee Yahwe, uje mahali pako pa kupumzika, wewe na sanduku la nguvu zako!
9Makuhani wako na wavikwe uadilifu; waaminifu wako washangilie.
10Kwa ajili ya mtumishi wako Daudi, usimuache mfalme wako uliye mpaka mafuta.
11Yahwe alimwapia Daudi kiapo cha uhakika, kiapo cha uhakika ambacho hatakivunja: “Nitamuweka mmoja wa wazawa wako kwenye kiti chako cha enzi.