1Msaada, Yahweh, kwa kuwa wacha Mungu wametoweka; nao waaminifu wametokomea.
2Kila mmoja anasema kwa jirani yake maneno matupu; kila mmoja anaongea kwa midomo yenye sifa za uongo na maneno ya udanganyifu.
3Yahweh, katilia mbali midomo yenye sifa za uongo, kila ulimi unanena kwa nguvu mambo makubwa.