61Kamba za waovu zimenifunga; nami sijaisahau sheria yako.
62Katikati ya usiku ninaamka kukushukuru wewe kwa sababu ya amri za haki yako.
63Ninaurafiki na wale wanao kuabudu wewe, wale wote watiio maagizo yako.
64Yahwe, nchi, imejaa uaminifu wa agano lako; unifundishe sheria zako. TETH.
65Wewe umemtendea mema mtumishi wako, Yahwe, sawasawa na neno lako.
66Unifundishe utambuzi sahihi na uelewa, kwa kuwa nimeamini katika amri zako.
67Kabla sijateswa nilipotea, lakini sasa nimelitii neno lako.
68Wewe ni mwema, na ndiye yule utendaye mema; unifundishe sheria zako.
69Wenye kiburi wamenichafua kwa uongo, lakini niliyashika maagizo yako kwa moyo wangu wote.
70Mioyo yao ni migumu, lakini ninafurahia katika sheria yako.
71Ni vizuri kwangu kuwa nimeteseka ili niweze kujifunza sheria zako.
72Maagizo yatokayo kinywani mwako ni ya thamani zaidi kwangu kuliko maelfu ya vipande vya dhahabu na fedha. YOD.
73Mikono yako imeniumba na kunitengeneza; unipe uelewa ili niweze kujifunza amri zako.
74Wale wanao kucha wewe watafurahi wanionapo kwa sababu ninapata tumaini katika neno lako.
75Ninajua, Yahwe, kuwa amri zako ni za haki, na kuwa katika uaminifu ulinitesa.
76Agano lako aminifu na linifariji, kama ulivyomwahidi mtumishi wako.
77Unihurumie ili niweze kuishi, kwa maana sheria yako ni furaha yangu.
78Wenye kiburi na waaibishwe, maana wamenitukana; bali mimi nitayatafakari maagizo yako.
79Wale wote wanao kucha wewe na wanigeukie, wale wazijuao amri za agano lako.
80Moyo wangu uwe mkamilifu pamoja na heshima kwa sheria zako ili nisiaibike. KAPH.
81Ninazimia kwa kutamani sana kuwa wewe unaweza kuniokoa! Ninamatumaini katika neno lako.
82Macho yangu yanatamani sana kuiona ahadi yako; ni lini utanifariji mimi?
83Kwa maana nimekuwa kama kiriba katika moshi; sisahau sheria zako.
84Ni kwa muda gani gani mtumishi wako atalazimika kuyavumilia haya; ni lini utawahukumu wale wanaonitesa?
85Wenye kiburi wamenichimbia shimo, wasiotii sheria yako.
86Amri zako zote ni za kuaminika; wale watu walinitesa bila ya haki; unisaidie.
87karibu kunifanya nifikie mwisho juu ya nchi hii, lakini siyakatai maagizo yako.
88Kwa upendo wako thabiti, uniweke hai, ili niweze kuzitii amri zako. LAMEDH.