165Wana amani nyingi, waipendao sheria yako; hakuna cha kuwatia mashakani.
166Naungoja wokovu wako, Yahwe, na ninatii amri zako.
167Ninazishika amri zako thabiti, na ninazipenda sana.
168Ninayashika maagizo yako na amri zako thabiti, kwa maana unajua kila kitu nifanyacho. TAV.
169Sikia kilio changu, Yahwe; unipe uelewa wa neno lako.
170Maombi yangu yaje mbele zako; unisaidie, kama ulivyoahidi katika neno lako.
171Midomo yangu na imwage sifa, maana wewe unanifundisha sheria zako.
172Ulimi wangu na uimbe kuhusu neno lako, maana amri zako zote ni za haki.
173Mkono wako unisaidie, maana nimechagua maagizo yako.