Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi

Zaburi 2

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Kwa nini mataifa wanafanya dhoruba, kwa nini watu wanafanya njama ambazo zitafeli?
2Wafalme wa nchi kwa pamoja hushikilia misimamo yao na watawala kwa pamoja hufanya njama kinyume na Yahwe na kinyume na Masihi, wakisema,
3“Ngoja tuzikate pingu walizo tufingia sisi na kuzitupa pingu zao.”
4Yeye aketie katika mbingu atacheka kwa dharau mbele yao; Bwana atawadhihaki wao.
5Kisha ataongea nao katika hasira yake na kuwaogofya kwa gadhabu yake, akisema,
6“Mimi mwenyewe nilimpaka mafuta mfalme wa Sayuni, mlima wangu mtakatifu.”
7Nami nitatangaza amri ya Yahwe. Yeye aliniambia, “wewe ni mwanangu! Leo hii nimekuwa baba yako.
8Uniombe, nami nitakupa wewe taifa kwa ajili ya urithi na mikoa ya nchi iliyo bora kwa ajili ya umiliki wako.
9Wewe utawavunja wao kwa fimbo ya chuma; kama vile mtungi wa mfinyanzi, wewe utawavunja wao vipande vipande.”
10Hivyo sasa, ninyi wafalme; mchukue tahadhari; mjirekebishe.
11Mwabuduni Yahwe kwa hofu na mfurahi mkitetemeka.
12Mumbusu mwana vinginevyo atawakasirikia, na mtakufa pale pale hasira yake ikiwaka. Ni jinsi gani wamebarikiwa wale wote watafutao usalama ndani yake.