Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Ayubu

Ayubu 34

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Zaidi ya hayo, Elihu aliendelea kusema:
2“Sikilizeni maneno yangu, ninyi watu wenye hekima; nisikieni, ninyi mlio na maarifa.
3Kwa kuwa sikio huyajaribu maneno kama ambavyo kaakaa huonja chakula.
4Na tujichagulie sisi wenyewe yale yenye adili: na tujigundulie miongoni mwetu yale yaliyo mazuri.
5Kwa kuwa Ayubu amesema, 'mimi ni mwenye haki, lakini Mungu ameondoa haki zangu.
6Pamoja na haki zangu, ninaangaliwa kama mwongo. Kidonda changu hakiponyeki, ingawa mimi sina dhambi.'
7Ni mtu gani aliye kama Ayubu ambaye hunywa dharau kama maji,
8ambaye huzunguka katika ushirika wa watu ambao ni waovu, na ambaye hutembea pamoja na watu waovu?
9Kwa kuwa anasema, 'Hakuna faida kwa mtu kujifurahisha kwa kufanya mambo ambayo Mungu anayataka.'
10Basi nisikilizeni mimi, enyi watu wenye ufahamu: na iwe mbali na Mungu kwamba atatenda uovu;
11na iwe mbali na Mwenye enzi kwamba atatenda dhambi. Kwa kuwa humlipa mtu kutokana na kazi yake; na humfanya mtu apate thawabu za njia zake mwenyewe.
12Kwa hakika, Mungu hatendi uovu, wala Mwenye nguvu hajaIpotosha haki.
13Ni nani aliyemweka kuwa mtawala wa dunia? Ni nani aliyeiweka dunia yote chini yake?
14Ikiwa aliweka makusudio yake juu yake mwenyewe, na kama amejikusanyia mwenyewe nafsi yake na pumzi yake,
15basi miili yote itateketea pamoja; mwanadamu angerudi mavumbini tena.
16Kama sasa mna ufahamu, sikilizeni haya; sikilizeni sauti ya maneno yangu.
17Je yeye anayeichukia haki aweza kutawala? Je mtamhukumu Mungu kuwa ni mwenye makosa, ambaye ni mwenye haki na mwenye nguvu?
18Mungu ambaye humwambia mfalme, 'Wewe ni mbaya; au huwaambia wenye kuheshimiwa, 'Ninyi ni waovu'?

19Mungu ambaye haoneshi upendeleo kwa viongozi na ambaye hawakubali zaidi watu matajiri kuliko masikini, kwa kuwa wote ni kazi ya mikono yake.
20Watakufa kwa muda mfupi; wakati wa usiku watu watatikiswa na watapita; watu wenye nguvu watatwaliwa mbali, lakini si kwa mikono ya wanadamu.
21Kwa kuwa macho ya Mungu yako juu ya njia za mtu; anaziona hatua zake zote.
22Hakuna giza, wala hakuna weusi mzito ambao watenda mabaya wanaweza kujificha wao wenyewe.
23Kwa kuwa Mungu hahitaji kumchunguza mtu zaidi; wala hakuna haja kwa mtu yeyote kwenda mbele zake kwa hukumu.
24Huwavunja vipande vipande watu wenye nguvu kwa ajili ya njia zao ambazo hazihitaji uchunguzi zaidi; huwaweka watu wengine katika nafasi zao.
25Kwa namna hii ana maarifa juu ya matendo yao; huwatupa watu hawa wakati wa usiku; nao wameangamizwa.
26Huwaua kwa matendo yao mabaya kama wakosaji dhahiri mbele za watu wengine
27kwasababu wamegeuka na kuacha kumfuata yeye na wamekataa kuzisadiki njia zake zozote.
28Na kwa namna hii, wamekifanya kilio cha watu masikini kimfikie; amekisikia kilio cha watu walioteswa.
29Na wakati akaapo kimya, nani aweza kumhukumu kuwa mkosaji? Kama akiuficha uso wake, ni nani awezaye kumjua? Anatawala sawa sawa juu ya taifa na mtu pia,
30ili kwamba watu wasiomjua Mungu wasije wakatawala, ili kwamba asiwepo mtu wa kuwanasa watu.
31Fikiria mtu akimwambia Mungu, 'Mimi ni mwenye hatia kabisa, lakini sitatenda dhambi tena;
32nifunze kile ambacho siwezi kukiona; nimetenda dhambi, lakini sitafanya tena.'
33Je unadhani kwamba Mungu ataiadhibu dhambi ya mtu huyo, kwa kuwa unayachukia yale ambayo Mungu huyatenda? Ni lazima uchague, siyo mimi. Basi sema yale ambayo unayajua.
34Watu wenye ufahamu wataniambia, kwa kweli, kila mtu mwenye hekima ambaye hunisikia atasema,
35Ayubu anazungumza bila maarifa; maneno yake hayana hekima.'
36Kama Ayubu alijaribiwa kwa kitu kidogo kabisa katika kesi yake kwasababu ya kuongea kwake kama watu waovu.

37Kwa kuwa anaongeza uasi juu ya dhambi yake; anapiga makofi ya dharau kati yetu; anaweka maneno kinyume na Mungu.”