Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Ayubu

Ayubu 22

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Kisha Elifazi Mtemani akajibu na kusema,
2Je mtu anaweza kumfaa Mungu “Je mwenye hekima anaweza kufaa kwake.
3Je inafurahisha kwa Mwenyezi ikiwa u mwenye haki? Je ni faida yake ukiyafanya safi maisha yako?
4Je ni kwa sababu ya uchaji wako kwake hata akukemee na kukuadhibu?
5Je si kwa sababu ya wingi wa uovu wako? Je hakuna mwisho wa makosa yako?
6Kwa maana umechukua dhamana kutoka kwa ndugu yako bila sababu; umechukua mavazi ya mtu na kumwacha uchi.
7Haukuwapa wenye kiu maji ya kunywea; umewanyima chakula wenye njaa
8japokuwa wewe, mwenye uwezo, uliimiliki nchi, japokuwa wewe, mwenye kuheshimiwa, uliishi ndani yake.
9Umewaacha wajane waondoke bila kitu; umewatesa yatima.
10Kwa hiyo, mabaya yanakuzunguka, na hofu za ghafla zinakusumbua.
11Kuna giza, hata usione; gharika inakufunika.
12Je Mungu hayupo juu mbinguni? Anaangalia juu ya nyota, jinsi zilivyo juu!
13Unasema, 'Mungu anajua nini? Je anaweza kuamua kupitia giza totoro?
14Mawingu ni kifuniko chake, hata asituone; anatembea anga la mbinguni.'
15Je utayaishi maisha ya zamani walioishi waovu -
16walioondolewa kabla ya siku zao, ambao misingi yao imeondolewa kama mto,
17waliomwambia Mungu, 'Ondoka kwetu'; waliosema, 'Mwenyezi anaweza kututenda nini?
18Hata hivyo bado alizijaza nyumba zao kwa mema; mipango ya waovu iko mbali nami.

19Wenye haki wanayaona yawapatayo waovu na kufurahi; wasio na hatia wanawacheka kwa dhihaka.
20Wanasema, 'Bila shaka walioinuka kinyume chetu wameondolewa; moto umeteketeza mali zao.'
21Basi patana na Mungu na uwe na amani naye; kwa njia hiyo, mema yatakujia.
22Nakusihi, pokea, maelekezo yake; uyatii maneno yake.
23Ukimrudia Mwenyezi, utajengwa, ukiacha kutenda uovu makaoni mwako.
24Weka hazina zako mavumbini, dhahabu ya Ofiri kati ya mawe ya vijito,
25na Mwenyezi atakuwa hazina zako, fedha ya thamani kwako.
26Nawe utajifurahisha katika Mwenyezi; utamwangalia Mungu.
27Utamwomba, naye atakusikiliza; utamtolea nadhiri.
28Lakini pia utatamka lolote, nawe utapewa; nuru itaangaza maishani mwako.
29Mungu humshusha mwenye kiburi, naye humwinua mnyenyekevu.
30Atamwokoa asiye na hatia; utaokolewa kupitia usafi wa mikono yako.”