5Mwimbieni Yahwe sifa kwa kinubi, kwa kinubi na wimbo wenye muiki wa kupendeza.
6Kwa panda na sauti ya baragumu, fanyeni kelele za shangwe mbele ya Mfalme, Yahwe.
7Bahari na ipige kelele na vyote vilivyomo, ulimwengu na wale wakaao ndani yake!
8Mito na ipige makofi, na milima ipige kelele kwa furaha.
9Yahwe anakuja kuihukumu nchi; naye ataihukumu dunia kwa haki na mataifa kwa adili.