8Tambueni, ninyi watu wajinga! Enyi wapumbavu, mtajifunza lini?
9Yeye aliye liumba sikio, hasikii? Yeye aliye litengeneza jicho, haoni?
10Yeye awaadhibuye mataifa, hayuko sahihi? Yeye ndiye ampaye maarifa mwanadamu.
11Yahwe anayajua mawazo ya wanadamu, kuwa ni mvuke.
12Amebarikiwa yule ambaye umuongozaye, Yahwe, yule ambaye wewe humfundisha kutoka katika sheria yako.