24Kweli yangu na uaminifu wa agano vitakuwa pamoja naye; kupitia jina langu atakuwa mshindi.
25Nitaweka mkono wake juu ya bahari na mkono wake wa kuume juu ya mito.
26Yeye ataniita, 'Wewe ni Baba yangu, Mungu wangu, na mwamba wa wokovu wangu.'
27Nitamjalia kuwa kama mzaliwa wangu wa kwanza, aliye inuliwa zaidi juu ya wafalme wa nchi.
28Nitaongeza uaminifu wa agano langu kwake milele; na agano langu pamoja naye litakuwa salama.
29Nitaufanya uzao wake kudumu milele na kiti chake cha enzi kitadumu kama mbingu zilizo juu.
30Ikiwa watoto wake wataziacha sheria zangu na kutokutii amri zangu,
31na kama watazivunja sheria zangu na kutokuzishika amri zangu,
32ndipo nitauadhiu uasi wao kwa fimbo na uovu wao kwa makofi.
33Lakini sitauondoa kwake upendo wangu thabiti wala kutokuwa mwaminifu kwa ahadi yangu.
34Sitavunja agano langu wala kubadilisha maneno ya midomoni mwangu.
35Mara moja na kwa yote, nimeapa kwa utakatifu wangu sitamdanganya Daudi:
36uzao wake utaendelea milele na kiti chake cha enzi kama vile jua mbele yangu.
37Kitaimarishwa milele kama mwezi, shahidi mwaminifu mawinguni.” Selah
38Lakini wewe umemtupa na kumkataa; umemkasirikia mfalme mpakwa mafuta wako.
39Wewe umelikataa agano la mtumishi wako. Umeinajisi taji yake ardhini.
40Umevunja kuta zake zote. Umeharibu ngome yake.
41Wapita njia wote wamemuibia, amekuwa kitu chenye kinyaa kwa majirani zake.
42Umeinua mkono wa kuume wa adui zake; umewafurahisha adui zake wote.
43Umeyageuza makali ya upanga wake. Na hukumfanya asimame awapo vitani.
44Umeimaliza fahari yake; umekitupa ardhini kiti chake cha enzi.