16Siku zote wanafurahia katika jina lako, na katika haki yako wanakutukuza wewe.
17Wewe ni fahari ya nguvu zao, na kwa nguvu zako tu washindi.
18Maana ngao zetu ni za kwako Yahwe; mfalme wetu ni wa Mtakatifu wa Israeli.
19Muda mrefu uliopita ulizungumza na waaminfu wako katika maono; ulisema, “Nimeweka taji juu ya mwenye nguvu; nimemuinua aliyechaguliwa kutoka kati ya watu.
20Nimemchagua Daudi mtumishi wangu; kwa mafuta yangu matakatifu nimempaka yeye.
21Mkono wangu utamsaidia yeye; mkono wangu utamtia nguvu.
22Hakuna adui atakaye mdanganya; hakuna mwana wa uovu atakaye muonea.
23Nitawaangamiza adui zake mbele yake; nitawaua wale wamchukiao.
24Kweli yangu na uaminifu wa agano vitakuwa pamoja naye; kupitia jina langu atakuwa mshindi.
25Nitaweka mkono wake juu ya bahari na mkono wake wa kuume juu ya mito.
26Yeye ataniita, 'Wewe ni Baba yangu, Mungu wangu, na mwamba wa wokovu wangu.'
27Nitamjalia kuwa kama mzaliwa wangu wa kwanza, aliye inuliwa zaidi juu ya wafalme wa nchi.