7Gadhabu yako yanielemea, na mawimbi yako yote yanatua juu yangu. Selah
8Kwa sababu yako, wale wanijuao wote hunikwepa. Umenifanya wakutisha machoni pao. Nimefungwa na siwezi kutoroka.
9Macho yangu yamefifia kutokana na shida; kila siku nakuita wewe, Yahwe; ninakunyoshea wewe mikono yangu.
10Je! utafanya miujiza kwa ajili ya wafu? Wale waliokufa watafufuka na kukusifu wewe? Selah
11Uaminifu wa agano lako utatangazwa kaburini? au uaminifu wako mahali pa wafu?