7Katika siku ya shida ninakuita wewe, kwa maana utanijibu.
8Katikati ya miungu hakuna wa kufananishwa na wewe, Bwana. Hakuna matendo kama matendo yako.
9Mataifa yote ambayo umeyafanya yatakuja kwako na kusujudu mbele zako, Bwana. nao wataliheshimu jina lako.
10Kwa kuwa wewe ni mkuu na utendaye mambo ya ajabu; wewe pekee ndiwe Mungu.
11Unifundishe njia zako, Yahwe. Kisha nitatembea katika kweli yako. Unifanye kukuheshimu wewe.
12Bwana Mungu wangu, nitakusifu kwa moyo wangu wote; nitalitukuza jina lako milele.
13Kwa maana uaminifu wa agano lako ni mkuu kwangu; wewe umeokoa uhai wangu kutoka chini kuzimuni.
14Ee Mungu, wenye kiburi wameinuka dhidi yangu. Kundi la watu wenye vurugu wanautafuta uhai wangu. Nao hawakuheshimu wewe.
15Lakini wewe, Bwana, ni mwenye huruma na neema, hukasiliki haraka, na mwingi katika uaminifu wa agano lako na kweli.
16Unigeukie na unihurumie; mpe nguvu zako mtumishi wako; umuokoe mwana wa mjakazi wako.