7Katika siku ya shida ninakuita wewe, kwa maana utanijibu.
8Katikati ya miungu hakuna wa kufananishwa na wewe, Bwana. Hakuna matendo kama matendo yako.
9Mataifa yote ambayo umeyafanya yatakuja kwako na kusujudu mbele zako, Bwana. nao wataliheshimu jina lako.
10Kwa kuwa wewe ni mkuu na utendaye mambo ya ajabu; wewe pekee ndiwe Mungu.
11Unifundishe njia zako, Yahwe. Kisha nitatembea katika kweli yako. Unifanye kukuheshimu wewe.