5Aliitoa kama maelekezo kwa Yusufu alipoenda katika nchi ya Misri, ambako nilisikia sauti ambayo sikuweza kuitambua:
6“Niliutua mzigo kutoka mabegani mwake; mikono yake ilipumzishwa kubeba kikapu.
7Katika dhiki yako uliniita, nami nikakusaidia; nilikujibu kutoka katika wingu jeusi la radi. Nilikujaribu kwenye maji ya Meriba. Selah