61Aliruhusu nguvu zake kutekwa na kuutoa utukufu wake mkononi mwa adui.
62Aliukabidhi upanga watu wake, na aliukasirikia urithi wake.
63Moto uliwavamia vijana wao wa kiume, na vijana wao wa kike hawakuwa na nyimbo za harusi.
64Makuhani wao waliangushwa kwa upanga, na wajane wao hawakulia.
65Kisha Bwana aliamshwa kama aliyetoka usingizini, kama shujaa apigaye kelele kwa sababu ya mvinyo.
66Aliwarudisha adui zake nyuma; aliwaweka kwenye aibu ya milele.
67Aliikataa hema ya Yusufu, na hakulichagua kabila la Efraimu.
68Alilichagua kabila la Yuda na Mlima Sayuni aliyoupenda.
69Alipajenga patakatifu pake kama mbinguni, na kama nchi aliyoiimarisha milele.
70Alimchagua Daudi, mtumishi wake, alimchukua kutoka zizi la kondoo.
71Alimtoa kutoka katika kufuata kondoo pamoja na wana wao, na kumweka kuwa mchungaji wa Yakobo, watu wake, na Israeli, urithi wake.